Pre-Form 1

Share

Tumeanza kupokea maombi ya kozi ya Pre-Form 1 kwa wanafunzi ambao watamaliza darasa la saba 2024 na wanatarajia kuanza kidato cha kwanza mnamo January 2025.

Kozi yetu ya Pre-Form 1 itadumu kwa wiki 8 ikijumuisha: makazi na chakula, masomo ambayo ni Kiingereza, Hisabati, Sayansi, Mafunzo ya Tarakilishi na masomo ya ziada ya ujuzi wa Maisha.

Mpango huu ni bure kabisa hakuna malipo yoyote kwa watoto waliokidhi moja ya vigezo vifuatavyo:

  • Watoto ambao ni yatima au wametengwa (baba au wazazi wote wamekufa au wazazi wote wamemtelekeza mtoto).
  • Watoto wa mitaani au wana hali duni.
  • Watoto ambao wameteseka au wako katika hatari ya kunyanyaswa, kupuuzwa au kunyonywa.

Mwisho wa kozi hiyo, baadhi ya wanafunzi watachaguliwa kwa udhamini kamili kutoka kidato cha 1 hadi kidato cha 4.

Ukitaka kupakua/download fomu ya maombi  bofya hapa.

Tuma maombi kwa kupitia: preform1@kijana-kwanza.org au WhatsApp: 0754 544 203.

Mwisho wa kutuma maombi haya ni Jumapili, 30 Juni 2024.