MDHAMINI:BABA SHIRAZ.
Advera ni msichana mkimya mpole mwenye nidhamu sana anayeheshimu kila mtu hupenda kujitenga sio mtu wa kujichanganya sana na wenzake.
Hupenda sana kujishughulisha na kazi za nyumbani kama vile kupika, kuosha vyombo na nyingine kama hivyo, Advera hushiriki vizuri kama suala zima la kidini na hivyo huhitaji kukumbushwa kuhusu dini.
AFYA
Alipata tatizo na fungus pamoja na UTI na alipatiwa matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri kiafya. Hujitahidi sana katika kuhakikisha kuwa anatumia muda wake vizuri katika shughuli zake na pia huhudhuria vipindi vya jioni ipasavyo bila kuwa na msukumo wowote.
Hushiriki katika vipindi vya njee darasani ambavyo humsaidia sana yeye kuwa karibu na wenzake na ameonekana kufurahia sana vipindi hivi humfanya yeye kuongeza maarifa na kuweza kukabiliana na changamoto katika Maisha yake.
Ameimarika sasa katika suala la usafi tofauti na kipindi cha nyumba sasa anao uwezo wa kujisimamia mwenyewe kufanya usafi wake binafsi na usafi wa mazingira.
Anaweza kutunza mali zake pamoja na mali za taasisi hata ikitokea mwenzake wameacha` au kutokutunza vitu vyao yeye huwahifadhia na kuwapatia inapotokea muhitaji.
Ana uwezo wa kudhibiti hasira zake hata inapotokea mtu kumuudhi au kupishana kauli yeye huwa habishani huwa ana kaa kimya kwani ndio njia pekee ya kuweza kustahamili hasira zake.
Amekua kimya sana kiasi kwamba inachukua muda sasa kuweza kumuelewa au kumsaidia.
Imeandikwa na Aziza Adam (msimamizi wa Wanafunzi)